Habari za Mastaa

The Game akimbia deni la Dola Milioni 7, Mahakama yatoa maagizo

on

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa Rapper The Game amekuwa akimkwepa mwanadada Priscilia Rainey baada ya kudaiwa kiasi cha dola za Kimarekani Mil 7.4 kama fidia la kosa lake kwa kumnyanyasa kingono mwanadada huyo mapema mwaka huu 2019.

Imeelezwa kuwa The Game ameonekana kukimbia deni lake na kutolikamilisha kwa wakati hivyo imemlazimu Jaji Mkuu mjini Los Angeles kutoa maamuzi na kumruhusu Priscilla kuzuia mapato yoyote yatakayoingia kutoka kwenye label ya muziki ya rapper huyo ikiwemo na haki zote kutoka kwenye makampuni pamoja na benki zake zote.

Hata hivyo Jaji ametoa onyo na kusema kuwa endapo The Game ataenda kinyume kwa kushindwa kulipa fedha hizo basi itamlazimu kumfikisha kizimbani kwa kosa la kuidharau Mahakama.

VIDEO: SHULE ILIYOONGOZA KIDATO CHA SITA, SKENDO YA BANGI, WIZI WA MITIHANI VYAZUNGUMZWA

Soma na hizi

Tupia Comments