Habari za Mastaa

Hawa ndio aina ya wanawake anaovutiwa nao msanii A.K.A kutoka South Africa!!

on

AKA Worldwide 2

A.K.A (A.K.A Worldwide) ni msanii maarufu kutoka Cape Town South Africa ambae miezi michache iliopita alialikwa jijini Dar es salaam kuperform kwenye party ilioshika headlines kubwa; Zari All White Party. Msanii huyu anafahamika kwa hit songs zake kama Congratulate na All Eyes on Me aliomshirikisha msanii Burna Boy kutoka Nigeria. 

Nimekutana na interview moja aliofanya msanii huyu nchini Nigeria na moja kati ya maswali alioulizwa A.K.A ni kuhusiana na aina ya wanawake anaovutiwa nao. Najua watu wengi watasema labda wanavutiwa na sura au umbo la mwanamke lakini mtazamo wa A.K.A ni tofauti kidogo, yeye alikua na haya ya kusema:

A.K.A >>> “Wanawake wanaonivutia mimi sio wenye sura nzuri sana wala umbo zuri sana bali wenye upeo wa kuona mbali, mtu ambae haishi ili mradi tuu bali anaishi kwa malengo, pia mimi zivutiwi na wanawake ambao hawanipi msukumo wowote ule maishani mwangu, navutiwa na mwanamke ambae ana msukumo wa kufanya vitu vikubwa kwa sababu kwa dunia tunayoishi sasa kama huna ndoto za mbali usitegemee utakua na mwanamke ambae ana mawazo hayo pia, ukweli huo pia upo kwa wanawake vile vile”.

Swali lingine aliloulizwa lilikua kama angepewa nafasi ya mwisho kuperform nyimbo yoyote ya kwake duniani, angechagua kuperform nyimbo gani na kwanini?

A.K.A >>> “Duuh! kama ningepewa nafasi ya kuperform mara ya mwisho duniani basi ningeperform nyimbo yangu ya Congratulate kwasababu ni nyimbo nilioiandika wakati ambao nilikaa na kutazama nilipotoka na kuona kua nimepiga hatua nzuri kimuziki kwani muziki wangu ulikua umeanza kutoka na kupigwa katika nchi mbali mbali za Affrica, kwangu kitu hicho kilikua na hatua ya mafanikio, so nikaamua kutoa nyimbo kujipongeza.”

Hapa chini nimekusogezea videos za hit songs zake Congratulate na All Eyes on Me.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments