Habari za Mastaa

Hatimae Kanye & Kim Kardashian wampokea mtoto wa nne

on

Inaelezwa kuwa Kim Kardashian pamoja na mume wake Kanye West wamebahatika kupata mtoto wa 4 muda mchache uliopita leo May 10,2019, jinsia ya mtoto huyo wa kiume na amepatikana kwa njia ya Mama mbadala (Surrogate Mother).

Inaripotiwa kuwa jina la mtoto huyo wa kiume ni Robert Harut, Kanye West pamoja na Kim Kardashian itakuwa ni mara yao ya pili kutumia njia hiyo ya kumpandikiza mama mbadala yaani “Surrogate mother” mtoto wao wa tatu ambaye ni Chicago West alizaliwa kwa njia hiyo pia.

Kanye West akiwa na mke wake pamoja na watoto wake

Kim Kardashian alipata matatizo ya uzazi baada ya kujifungua mtoto wake wa pili Saint west hiyo ni taarifa iliyotolewa na Daktari wake na kusema kuwa endapo atapata ujauzito mwingine basi unaweza ukatahatarisha maisha yake, ndio maana kwa mtoto wao wa tatu na nne wametumia njia mbadala.

Kupitia ukurasa wa twiter Kim Kardashian aliandika “Ni pacha wa Chicago, nina uhakika atabadilika lakini kwa sasa anafanana nae, yupo hapa tayari na ni mkamilifu”

VIDEO: Ommy Dimpoz bado anajiuliza “Ni mimi kweli?”, RIP Dr. Mengi

Soma na hizi

Tupia Comments