Habari za Mastaa

Mtoto wa R. Kelly aacha shule kisa ada

on

Inaelezwa kuwa mtoto wa  mwimbaji R. Kelly, Joann Lee ameripotiwa kufukuzwa chuo kutokana na kutolipa ada. Lee ambaye anasoma chuo cha sanaa huko Jijini Calfornia Marekani alijikuta anarudishwa nyumbani kwa kushindwa kulipa ada kwa wakati baada ya kufika na kutoruhusiwa kuingia.

Inadaiwa kuwa Meneja wa R. Kelly, Darrell Johnson ametoa taarifa kuwa msanii huyo hakushindwa kulipa fedha hizo ila asimamisha zoezi hilo baada ya kupata taarifa za Joann kuacha chuo mwaka 2018. R.Kelly amekuwa tayari kulipa lakini mpaka atakapo oneshwa kweli pesa zinahitajika kwa mfumo wa Bill statements.

Inaripotiwa kuwa hakuna maelewano mazuri kati ya R.Kelly na binti yake huyo toka kuachiwa kwa makala ya “Surviving R.Kelly” na kudaiwa kuwa R.Kelly amekuwa akimtupia lawama mama wa mtoto huyo na kdai kuwa anampandikiza chuki binti yake.

VIDEO: ULIPITWA NA MAJIBU YA LINAH BAADA YA KUULIZWA ANAMZUNGUMZIAJE AMINI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments