Habari za Mastaa

Rasmi Brad Pitt na Angelina Jolie wamepeana talaka

on

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa Mwigizaji Brad Pitt kutokea Holly Wood pamoja na Mke wake Angelina Jolie wameachana rasmi baada ya kuripotiwa kuwa Angelina kudai talaka mwaka 2016.

Inaelezwa kuwa kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama, imeelezwa kuwa wawili hao walikamilisha shughuli za talaka Ijumaa ya April 12,2019 wikiendi iliyopita na kuelezwa kuwa kwa sasa wamepewa nafasi ya makubaliano kuhusiana na mali ikiwemo na malezi ya watoto wao 6.

Fahamu kuwa Brad Pitt na Angelina Jolie walifunga ndoa mwaka 2014 na wameshiriki kwenye filamu nyingi pamoja ikiwemo Mr & Mrs Smith, By The Sea na nyingine nyingi.

AUDIO: ULIPITWA NA HII YA NANDY KUMLILIA TENA RUGE? “NAKUMBUKA HII SIKU ULINISTUKIZA” BOONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA

Soma na hizi

Tupia Comments