Habari za Mastaa

Chris Brown aanza kumfuatilia Vanessa Mdee

By

on

Baada ya mwimbaji wa miondoko ya RnB Chris Brown kutangza kolabo yake na mkali wa Nigeria Davido Ijumaa ya July 12,2019 sasa huenda kukawa kuna nyingine kutokea hapa nyumbani hii ni baada ya CB kuonekana kum-follow Vanessa Mdee kwenye instagram yake.

Vanessa Mdee amekuwa miongoni mwa wafuasi zaidi ya Elf 3 ambao Chris Brown anawa-follow kupitia ukurasa wake wa instagram, mashabiki wengi wameibuka na kudai kuwa huenda CB amevutiwa na uwezo wa Vee kwenye masuala ya muziki.

Inawezekana kuwa Vanessa Mdee ndio msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kuwa miongoni mwa wafuasi wa CB, kupitia Insta story Vanessa hakutaka kuificha good news hii alipost na kuandikaNina uhakika kuwa wote mnafahamu kuwa nampenda huyu kijana, Chris Brown anani-follow”

VIDEO: MAKONDA AFUNGUKA YA MOYONI SIKU YA BIRTHDAY YA MWANAE

Soma na hizi

Tupia Comments