Habari za Mastaa

Jay Z aingia kwenye biashara ya bangi (+Video)

on

Baada ya jarida la Forbes kumtaja Rapper Jay Z kuwa ndio msanii wa kwanza kwenye game la Hip Hop nchini Marekani  kufikia utajiri wa zaidi ya shilingi Trillioni 2 za Kitanzania kutokana na biashara zake sasa Jay Z ameamua kujikita kwenye biashara ya bangi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Rap Up umeripoti kuwa Jay Z ataungana na kampuni ya Caliva iliyopo mjini California Marekani kama mkuu wa mipango ya kampuni hiyo (Chief Brand Strategist) ambapo kazi yake kuu itakua kukuza na kuistawisha chapa ya kampuni ikiwemo kusaidia kushawishi kiuhalali watu kwenye kukuza kiwanda cha bangi.

Imeelezwa kuwa Jay Z ameungana na kampuni hiyo kwa mkataba wa miaka mingi mbeleni na ameungana na rappers kama Wiz Khalifa, Snoop Dogg, Rick Ross ambao wamejiingiza kwenye biashara hiyo ya bangi.

AUDIO: VERA SIDIKA KAJIBADILISHA RANGI, ERIC OMONDI ASHINDWA KUVUMILIA

Soma na hizi

Tupia Comments