Mix

Habari 5 kubwa kwenye TV za Tanzania April 27 2016

on

Kama utakua ni mpenzi wa kutazama taarifa ya habari na hukupata time ya kutazama taarifa ya Habari April 27 2016 kupitia TV za Tanzania usijali millardayo.com imekurekodia habari 5 kupitia TV za Tanzania.

Habari kutoka Channel 10Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka BRT

Watumiaji wa barabara watakiwa kuzingatia sheria za usalama barabrani ‘Hilo swala la watu wasio husika na miundo mbinu kutumia miundo mbinu, hiyo ndio hadha na kero ambazo tulizonazo sasa hivi kwa siku nne tu zilizopita  tayari magari yetu ya mradi yameshakwaruzana na watu wasiopaswa kutumia barabara hizi‘>>>Msemaji wa UDA RT
20160427_191906

Habari kutoka Clouds TVUstawi wa Watoto Upo Wapi

Walimwengu wanasema mtoto umleavyo ndio akuavyo iko wapi mantiki ya wazazi wanaowarekodi watoto wao, ‘Watoto wanavyofundishwa kitu chochote au wakafanyiwa matendo fulani yanaganda kwenye ubongo wao mpaka ukubwani  kwao‘>>>Mwanasaikolojia20160427_193339

Habari kutoka ITVMama Maria Nyerere Apongeza Serikali Kwa Kufanikisha Ujenzi wa Daraja la Kigamboni

Kwa bahati nzuri nashukuru mwenyezi Mungu amenipa maisha marefu kwasababu hili Daraja lilikuwa lijengwe tangu miaka hiyo ya kwanza na gharama zake walikadiria itakuwa sh. milioni 140 na wakati huo milioni 140 ilikuwa inaonekana ni pesa nyingi sana‘>>>Mama Maria Nyerer 20160427_201223

Habari kutoka ITVAthari za Mvua

Zaidi ya kaya 2000 hazina makazi Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki ameyaongea haya ‘kuanzia kule juu kote na huku ambapo  maji yamepita hakikisheni watu hawa wanahama, sasa niambiwa kuna shamba hapa ambalo limetelekezwa tangu miaka ya 70, nasema viongozi wa vijiji hakikisheni kuwa watu wote waliokuwa kwenye mapito ya maji wanajenga katika mashamba hayo‘>>> Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro20160427_200211

Habari kutoka Star TV...Taa za Kuongozea Magari

Wakazi wa Buzuruga Mwanza Wailalamikia SerikaliKusema kweli hizi taa ni jipu na lina hitaji kutumbuliwa juzi tu tumempoteza mwanamke mwenzetu aligongwa hapa na kupoteza maisha na pia mwanafunzi mwingine aligongwa hapahapa‘>>>Mkazi wa Buzuruga20160427_200653

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments