Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya September 13 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka ITV
Dar es salaam
kwa wahanga waliokumbwa na janga la tetemeko la ardhi mkoani kagera Serikali imetoa ombi kwa watu binafsi, makampuni na watanzania kiujumla kusaidia kuchangia wahanga hawa zaidi kupata makazi baada ya kubaini mpaka leo nyumba 840 zimeanguka mkoani hapo.
Habari kutoka Clouds TV
Bunge linaendelea mjini Dodoma na Kutokana na janga lililowakuta wenzetu wa Bukoba mkoani Kagera wabunge watoa posho zao za leo September 13 2016 na zimepelekwa kuchangia wahanga hao.
Habari kutoka ITV
BUNGENI DODOMA
Serikali yatoa taarifa juu ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi Kagera kuwa imeongezeka na kufikia idadi ya watu 17 mpaka sasa.
Habari kutoka Azam TWO
Sumu yazua taharuki Geita
Watu wa kijiji hicho wakumbwa na janga hilo baada ya sumu hiyo kuzagaa na kudhani kuwa ni peremende na kula na kudhurika na zaidi imepelekea wengine kupoteza maisha.
Habari kutoka Channel TEN
Wafugaji mkoani Simiyu watadhaharishwa
Wafugaji wa Simiyu watadhaharishwa kuwa mifugo yao iko hatarini kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa wanyama pori ambayo yanaweza kuwa na athari kwa mifugo yao.
ULIKOSA KUITAZAMA VIDEO YA MAMBO NANE YALIYOFANYWA NA SERIKALI BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI BUKOBA? UNAWEZA KUITAZAMA NIMEKUWEKEA HAPA CHINI