Habari zote zilizopewa airtime kwenye TV za Tanzania unazipata hapa mtu wangu Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya September 14 2016 usijali Millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari tano kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka ITV
Wakazi wa mkoa wa Kagera wamepewa tahadhari kwamba wanatakiwa kuendelea kuchukuwa tahadhari mpaka matetemeko mengine yatakapo tokea na kupunguza nguvu ndio ijulikane kwamba kunaweza kuwa na usalama lakini kwa sasa bado hali haijatengemaa.
Habari kutoka Clouds TV
Ukaguziwa magari utaanza rasmi September 26 2016 nchini kote na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘hatutaki ajali tunataka kuishi kwa usalama’.
‘Madereve wapeleke magari hayo matengenezo katika karakana zao na pindi yakikamilika watayajeresha tena kituoni kwajili ya ukaguzi wa pili‘- Kamanda usalama barabarani , DCP Mohammed Mpinga
Habari kutoka TBC1
Moto wateketeza hoteli ya kitalii Pwani, Kibaha Maili moja na umesababisha hasara kubwa hasa kuungua kwa mgahawa lakini shirika la zima moto kushirikiana na jesho la JWTZ wameshirikiana vyema kuzima moto huo.
Habari kutoka ITV
MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO
Taasisi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete yaingia kutoa huduma ya muda wa siku 5 kuhudumia watoto wenye matatizo ya moyo bure
Habari kutoka ITV
MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wameshakwisha kukopesha zaidi ya Trillion 2.4 na fedha zilizoko tayari kwa ajili ya kukusanya ni Billion 284 na licha ya kuanza kukusanya fedha hizo kwa mitandao ya simu wanalazimika kubadilisha sheria za mikopo ambapo sheria itamlazimu mwajiri kumkata mfanyakazi wake asilimia 15 tofauti ya asilimia 8 ya awali ili kurahisisha urejeshwaji wa mikopo hiyo.
ULIKOSA KUITAZAMA VIDEO YA BOT KUTOA UFAFANUZI JUU SHILINGI KUPANDA THAMANI AU KUSHUKA? UNAWEZA KUITAZAMA VIDEO NIMEKUWEKEA HAPA