Watu wenye umri wa kati yaani miaka 40 hadi 60 wanashauriwa kujenga tabia ya kutembea kwa mwendo mrefu na wa haraka haraka kuliko wale watu wenye umri mdogo ili kuimarisha afya zao na kuepuka matatizo ya afya na viungo.
Inaelezwa kuwa kutembea kwa haraka kwa umbali wa angalau dakika 10 huweza kupunguza hatari ya kifo cha mapema kwa asilimia 15% na inashauriwa kuwa watu wa umri huu wafanye shughuli za mwili za mazoezi kwa dakika 150 kwa wiki.
Mazoezi haya yanaelezwa kuwa na uwezo wa kurekebisha matatizo ya shinikizo la damu, uzito uliozidi, msongo wa mawazo, hisia za hofu na matatizo ya misuli na mifupa hususani maumivu ya mgongo na kiuno.
Uliiona hii? Baada ya kuonana na JPM, Rais wa JICA leo kawatembelea TANESCO