Upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya Sh bilioni 2.4
inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini, Archard Kalugendo na mwenzake upo katika hatua za mwisho kukamilika.
Mbali ya Kalugendo, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu.
Wakili wa serikali, Esther Martin amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kukamilisha taratibu zilizobaki.
Katika shauri lililopita, upande wa mashitaka ulidai kuwa kuna baadhi ya vitu vinapaswa kukamilishwa katika kesi hiyo ikiwemo kusubiri uamuzi kama ikasikilizwe Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ‘Mafisadi’ ama lah.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi January 31, 2018 kwa ajili ya kutajwa.
Kwa pamoja washitakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababisha serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 2.4.
Inadaiwa kuwa kati ya August 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababisha serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Watu 7 kizimbani kwa kujiunganishia bomba la mafuta ya Dizeli
Watuhumiwa wa ugaidi Arusha wavua nguo Mahakamani