Marais 10 warefu zaidi duniani, Afrika wapo wawili kwenye hii list..
Share
3 Min Read
SHARE
Kila siku watafiti wana habari mpya kuhusiana na maisha, tumeona tafiti nyingi zikifanywa zikiwemo za magari, majumba, watu maarufu.. Lakini sikuwahi kufikiri kwamba kuna siku nitakutana na utafiti unaozungumzia urefu wa Marais duniani.
Leo nakusogezea utafiti ambao ripoti yake ilitolewa January 4 2015 ambao unazungumzia marais 10 ambao ni warefu zaidi duniani:-
1. Filip Vujanovic
Papa Benedict xvi akiwa na Rais wa Montenegro ambaye ndiye rais mrefu kuliko wote duniani, ana urefu wa futi 6.5
2.Nicolas Maduro
Huyu ni Rais wa Venezuela, anashika nafasi ya pili kwa kuwa rais mrefu, ana urefu wa futi 6.3
3.Bashar Al- Assad
Huyu ndiye Rais wa tatu kwa urefu duniani kutoka Syria, ana urefu wa futi 6.2
4.Stephen Harper
Huyu ni Waziri mkuu wa Canada, ana urefu wa futi 6.2
5. Toomas Hendrik Ilves
Huyu ni rais wa Estonia ambaye pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari, ana urefu wa futi 6.2
6. Paul Kagame
Kwa Afrika huyu ndiye rais anayeongoza kwa urefu, lakini duniani anakamata nafasi ya sita kwa futi 6.2 huku binti yake akimzidi kwa kuwa na futi 6.6. Hapa Rais Kagame alikuwa na Rais Obamana mkewe.
7.Barack Obama
Barack Obamani Rais wa Marekani, ana urefu wa futi 6.1 huku mke wake Michelle Obama akiwa na futi 5.11
8.David Cameroon
Huyu ni Waziri mkuu wa Uingereza, urefu wake haujatofautiana na wa Rais Obamawa Marekani, wote wana futi 6.1
9.Blaise Compaore
Huyu alikuwa Rais wa Burkina Faso ambaye Oktoba mwaka jana aliamua kujiuzulu kutokana na machafuko nchini kwake, ana urefu wa futi 6. Hapa alikuwa na Rais Obama na wake zao.
10. Recep Tayyip Erdogan
Huyu ni rais wa Uturuki aliyekabidhiwa madaraka mwaka jana, ana urefu wa futi 6
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenyeFacebook,Twitter na Instagrampia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitterInstaFacebook