Mbunge wa Tarime Vijijini ‘CHADEMA’, John Heche amemtupia tuhuma Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga akidai amesaini mkataba wa uwekezaji kinyume cha sheria.
Heche amezungumza na waandishi wa habari leo April 12, 2017, na kusema licha ya Mkuu huyo wa Wilaya kusaini mkataba kinyume na sheria pia amekuwa akitumia nguvu na vitisho kwa wananchi wa eneo hilo kwa lengo la kupora ardhi yenye ukubwa wa hekta zaidi ya 34,000 ambayo hukaliwa na zaidi ya wakazi 30,000, kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha miwa.
“Wanakaa watu zaidi ya 30,000, hapo wanategemea hilo bonde; iwe kwa kilimo, iwe kwa kupata maji, iwe kwa samaki, iwe kwa ng’ombe wao kuchunga na maziwa, ni hilo bonde la Mto Mara.” – John Heche.
Bonyeza play hapa chini kutazama…
VIDEO: Majibu ya Waziri Nchemba kwa wanaosema amekaa kimya Kuhusu watu kutekwa. Bonyeza play kutazama.