HekaHeka

Hekaheka ya leo Feb 17, inahusu mtoto aliyefariki mazingira ya kutatanisha..

on

8452105488_7c7f02349eJumanne ya February 17, Hekaheka ya leo inahusu msichana wa kazi ambae aliachiwa mtoto na bosi wake ambae alikuwa anaumwa lakini hakuwa amezidiwa na baadae alipigiwa simu na jirani yake na kumueleza kuwa mtoto wake amefariki.

Mama wa mtoto amesema alienda Kariakoo akamwacha mtoto anacheza, akampa house girl maelekezo ya kumpa maziwa na dawa, alipofika Kariakoo alimpigia simu na kuulizia hali ya mtoto akamwambia anacheza na akamsikia kwenye simu.

Muda mfupi baadaye alipigiwa simu na jirani yake akimwambia kuwa mtoto amezidiwa, mama huyo akamuomba jirani amsaidie kumpeleka Hospitali, alipopigiwa tena mara ya pili alipewa taarifa kuwa mtoto amefariki.

Kilichomshangaza ni kuwa baada ya msiba msichana huyo alimfuata na kumwambia kuwa anamuonea huruma kwani kuna kitu kilimjia na kumwambia amzidishie mtoto dawa na asimpe chakula kisha amlaze chini ili kazi yao itimie,  mtoto akawa amefariki.

Msichana huyo alipoulizwa alisema kuwa alimpa mtoto dawa akafariki lakini amekuwa akioteshwa ndoto na ndugu zake na kuna kitu huwa kinamjia na kumtuma kumdhuru mtoto bila yeye kujijua, kwa sasa sura ya mtoto inamjia usiku na kumfanya akose usingizi.

Bonyeza play kusikiliza Hekaheka yote hapa.

https://soundcloud.com/millard_ayotv/hekaheka-feb-17-clouds-fmmp3

Unataka niwe nakusogezea kila kinachonifikia? Ungana na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia kila kitu moja kwa moja >>>Facebook Twitter Instagram

Tupia Comments