HekaHeka

Matonya na Tunda Man kwa pamoja kwenye Leo Tena @CloudsFM #Hekaheka…

on

Tonya & TundaKwenye Bongo Fleva ishu ya Tunda Man na Matonya kutokuwa na maelewano mazuri ni moja ya zilizosikika sana, kila mmoja alikuwa akilalamika tofauti kuhusu mwenzake, leo March 6 mastaa hao wamekutana kwa pamoja ndani ya studio za Clouds FM, wakati wa show ya Leo Tena.

Tunda Man amesema anachohisi alimkosea Matonya ni kusema kwamba alimtungia nyimbo lakini  hataki tena kuzungumzia ishu hiyo, amesema leo itakuwa mara ya mwisho kuzungumzia jambo hilo na kuomba radhi kwa yote yaliyotokea, hana tatizo lolote na Matonya.

Matonya amesema kuwa Tunda Man ni mdogo wake ambaye wamekutana vizuri na walikuwa wanaishi vizuri lakini alipata wasiwasi baada ya kuona kila siku kuna maneno yanaibuka ambayo hakupendezwa nayo, yeye binafsi anampenda Tunda Man na hata familia yake, kwa nafasi yake kama kaka ameamua kumsamehe.

Tunda amesema hawakuwahi kuonana tangu mwaka 2007.. Matonya akamalizia kwamba kwa sasa wako tayari kwa pamoja kuingia studio kufanya collabo.

tnda

Kusikiliza story yote ya Hekaheka bonyeza play hapa chini…

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments