HekaHeka

Kutana na nyumba ya maajabu Tanga ambayo watu wameshindwa kuishi ndani yake

on

Screen Shot 2014-08-21 at 2.48.22 PMNi wakati tuu tukiisubiria Serengeti Fiesta 2014 Jumamosi hii kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga na tukikutanishwa na wakali wa bongofleva tunaowakubali kama Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Nay wa Mitego, Young Killer, Stamina, Vanessa Mdee, Linah, Roma na wengine, tunaendelea kuyafahamu mengine ya Tanga.

Pengine umeshawahi kusikia stori kadhaa ambazo zinahusisha mkoa wa Tanga na maajabu yake, kuna ambayo nilishawahi kuisikia Tanga kuna wakati ukikipiga teke kifuu eti kinakusemesha kukwambia ukirudishe ulikokitoa.

Sasa Hekaheka ya Leo Aug 21 ni kutokea Tanga na inahusisha nyumba ambayo inasemekana watu wameshindwa kuishi kutokana na maajabu yaliyopo kwamba unaweza kulala peke yako halafu ukiamka unakuta umelala na paka.

Wapangaji kadhaa wameshindwa kuishi na mwenye nyumba katangaza kuuza lakini bado hajapata mteja, unaambiwa walinzi wa nyumba hiyo taa za usiku wanawasha mchana kwa kuhofia likiingia giza watakutana na mambo hayo.

Gea Habib kazungumza hadi na mlinzi aliyewahi kufanya kazi kwenye nyumba hiyo akizungumzia mazingira hayo magumu aliyowahi kukutana nayo ya kazi kwenye nyumba hiyo.

96.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tanga
Bonyeza play kusikiliza.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

Tupia Comments