HekaHeka

Mwanamke alipata ujauzito wakati mume wake yuko nje ya nchi, kingine kiko kwenye hii Hekaheka (Audio)

on

p14pregnantwomanGETTYv2

Kwenye #Hekaheka ya leo June 09 2015 kuna stori inayomhusu mama mmoja ambaye ni mke wa mwanajeshi, mwanamke huyo alipata ujauzito wa mtu mwingine wakati mume wake kasafiri nje ya nchi.

Wakati mwanaume anakaribia kurudi, huku nako mwanamke anakaribia kujifungua.. mwanamke akaona awatafute rafiki zake ambao ni mtu na mpenzi wake ili wamsaidie kumtunza mtoto huyo mume wake asijue.

Ishu ikawa walipoenda Ustawi wa Jamii ili waendelee na taratibu za kupata ruhusa ya kumtunza mtoto huyo, taarifa ikafika mpaka Polisi ambapo ilibidi mama wa mtoto huyo atafutwe.. Sehemu ya kwanza ya Hekaheka hiyo iko kwenye hii sauti hapa, mwendelezo wake utakuwa kwenye Leo Tena ya kesho @CloudsFM.

 

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments