HekaHeka

Hapa kuna Hekaheka iliyosikika kwenye Leo Tena @CloudsFM leo Jan 21, unaweza kuisikiliza (Audio)

on

torn piece of paper with divorce text and paper couple figures

millardayo.com hukuwekea Hekaheka za siku ili kama ulipitwa wakati ikiwa inaruka hewani kwenye Leo Tena ya Clouds FM, ukiingia hapa basi unapata nafasi ya kuisikiliza yote.

Ya leo January 21 inatoka Vingunguti Dar, mwanamke mmoja aliolewa na baadaye kuanza tabia ya kutomheshimu mume wake, siku moja alitoka na kurudi saa nne usiku akisema kuwa ametoka Clouds kuigiza na kuwataja Jackline Wolper na Wema Sepetu kuwa ndio wenyekiti wa kikundi chao cha maigizo.

Mume wake ameongea kwenye Hekaheka na kusema baada ya kuchoshwa na tabia hiyo aliamua kumpa talaka, kutokana na kutokana na kwamba hakupenda mke wake kujiingiza kwenye masuala ya uigizaji.

Hiz ni picha maharusi hao siku ya ndoa yao.

Hizi ni picha maharusi hao siku ya ndoa yao.

Mwanamke huyo alipoulizwa na Geah kuhusu ishu iliyofanya yeye na mumewe wametengana amesema kuwa mume wake hajaongea ukweli sababu ya wao kutengana kwa kuwa alikuwa anaondoka nyumbani asubuhi hamuachii hela ya kula hivyo akaamua kuondoka baada ya kupewa talaka.

Amesema kuwa kaamua kuondoka kwenda kufanya mambo yake mengine na sio kweli kwamba aliachwa kwa sababu ya kujiingiza kwenye uigizaji.

Hekaheka yote unaweza kuisikiliza hapa.

Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments