Leo kwenye Hekaheka ya @CloudsFM alikuwepo Ally Nipishe, moja ya jamaa ambao waliwahi kufanya poa kwenye Bongo Fleva alafu baadae akawa kimya hivi, viko vingi vilitokea katikati na sisi hatukujua kuhusu hilo, leo ametoa majibu yote.
Staa mwingine aliyekuwepo ni Pipi, jina lake liko kwenye list ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri pia kwenye Muziki TZ… Ally kasimulia vingi ikiwepo ishu ya mikasa mbalimbali iliyomkuta, kuna wakati alikamatwa akafungwa jela baada ya kuhusishwa na wizi wa pesa.
Ishu ilianzia pale alipouziwa gari, kumbe lilikuwa ni gari ambalo liliibiwa na ndani yake kulikuwa na pesa pia.. mpenzi wake alihusika pia kumuunganisha na waliomuuzia gari hilo.
Pipi naye amezungumzia mambo mengi, kumbe yeye na mpenzi wake wanatumia simu moja… yeye na mume wake wana misingi mizuri ya uaminifu, hawana mambo mengi kwa hiyo hawana sababu ya kufichana.
Nimekusogezea sauti yao hapa chini, bonyeza play kuisikiliza.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.