Heka heka ya leo inatoka maeneo ya Ilala, Dar es salaam, inahusu mama wa bibi harusi kulazimisha maharusi wakapime kwanza kabla ya kuondoka kwenda kuishi pamoja.
Kitendo cha mama wa bibi harusi na shangazi kulazimisha maharusi hao kwenda kupima kwa kulala mbele ya gari makusudi ili lisiondoke lilisababisha mvutano mkubwa miongoni mwa ndugu wa pande zote mbili ambao hawakuweza kufikia muafaka.
Baada ya mvutano mkubwa awali bwana harusi alikubali kwenda hadi Hospitali ya Amana kupima akiongozana na bibi harusi pamoja na ndugu wa pande zote mbili lakini walipofika gafla alikataa kupima kwa madai amedhalilishwa na kutaka arudishiwe fedha zake.
Inasemekana kuna mmoja wa watu aliwadokeza ndugu wa bibi harusi kuwa bwana harusi ni mgonjwa ingawa bw ana harusi amekiri tayari alishatembea na mke wake muda mrefu.
Isikilize hapa.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.