HekaHeka

Mwanamke alivyokimbiwa na mume baada ya kujifungua Muhimbili Dar… #Hekaheka (+Audio)

on

Hii stori imesikika kwenye show ya ‘Leo TenaClouds FM ambapo mwanamke mmoja amekimbiwa na mumewe baada ya kujifungua hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam.

Mwanamke huyo amesema baada ya kutoka hospitali alikuta mwanaume kabeba kila kitu kwenye nyumba walipokuwa wamepanga, akakosa msaada mpaka akajitokeza mama mmoja ambaye alimsaidia kumpa hifadhi kwa muda.

Japo wameishi pamoja kwa miaka mitatu, hajawahi kutambulishwa kwa ndugu zake kwa hiyo baada ya kumkimbia alikosa hata kwa kwenda kupata msaada wa  kumtafutia mume wake huyo.

Mama huyo amesema yuko kwenye wakati mgumu kiasi cha kufikiria kumtupa mtoto.

Hekaheka yenyewe hii hapa kwenye sauti yake

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments