Mix

Kisa mahindi ya kuchoma, Mume kamuunguza vibaya mke wake hadi kubaki mlemavu….#HekaHeka (Audio)

on

cry

HekaHeka ya leo inatoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbii ..kuna mama amefanyiwa vitendo vya ukatili na mume wake baada ya kuunguzwa vibaya na maji ya moto ya ugali na kumsababishia kukatwa ziwa moja.

Mama huyo kutoka Musoma ambaye ana watoto watatu amesema sababu kufanyiwa ukatili na mume wake alichuma mahindi mabichi mawili shambani kwao baada ya kusikia njaa na kuanza kuyachoma kitendo kilichomkasirisha mume wake.

Anasema wakati akimfanyia ukatili huo na mume wake, pia aliuweka mkono wake ndani ya moto na kusababisha ushindwe kufanya kazi kabisa na kuonekana kama mlemavu, pia alichelewa kwenda hospitali  baada ya kufungiwa ndani peke yake hali iliyosababisha vidonda vyake kuanza kuoza na kutoa funza.

Amesema kinachomuumiza zaidi ni mume wake huyo kuachiwa na kukimbia na mpaka sasa hajui hatma yake wala ya watoto wake.

Msikilize hapa.

HAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

Tupia Comments