HekaHeka

HekaHeka ya mwanamke asiye na kosa kuunguzwa na maji ya moto kisa wivu…(Audio)

on

hppp

HekaHeka ya leo inatokea hapa Dar es salaam baada ya dada mmoja kumuunguza mwenzake na maji ya moto ya ugali,,lakini aliyekuwa anamdhamiria kumbe si mwenyewe bali alikuwa shemeji wa mwanaume wake.

Eti alihisi ni mwanamke anayetembea na mpenzi wake baada ya kuona picha ya mtoto kwenye simu yake akidhani ndiye mama wa huyo mtoto.

Dada aliyeunguzwa ambaye ni mama mkubwa wa uyo mtoto anasema..uyo mtoto alikua akiumwa na wakafunga safari yeye na mama wa mtoto hadi kwa mwanaume ambaye aliacha kutoa huduma za malezi…na alipofika walimkuta na mama wa mtoto kuamua kumwachia mtoto wake.

Baada ya muda mwanamke ambaye alikua akiishi na mwanaume huyo alirejea nyumbani na kumkuta mama mkubwa wa mtoto baada ya mama yake kuondoka na akadhani ndiye mama wa mtoto na kuamua kuchukua maji ya moto na kumwangia mwilini.

Kwa sasa dada huyo amelazwa katika hospitali ya Palestina Sinza ikiwa ni wiki moja baada ya kufanyiwa unyama huo huku muhusika akishikiliwa na polisi.

Msikilize hapa…

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments