HekaHeka

HekaHeka ya mtoto kupotea wakati wa kujiandikisha kupigakura imesikika leo…Audio

on

bvr folen

Wakati zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa njia ya BVR likiendelea katika maeneo mbalimbali Dar kumekuwepo na matukio mbalimbali..jana Hekaheka ilizungumzia mama kupigwa na mume wake baada ya kuchelewa kumpikia.

Leo tena Hekaheka inazungumzia tukio la mtoto wa miaka mitatu kupotea wakati mama yake alipokwenda kujiandikisha maeneo ya Bunju.

Aliporudi nyumbani akamkuta mtoto mmoja mwingine hayupo na mara ya mwisho alionekana kwenye kituo cha daladala akiwa na dada mmoja.

Baadaye alipigiwa simu na mtu mmoja kutoka Mbezi ya Kimara na kuambiwa mtoto wake kapatikana kwa dada mmoja ambaye alidanganya jina la mtoto na kusema ni wa rafiki yake.

Isikilize hapa

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments