Hekaheka ya leo imetokea Mbagala Dar, Jumatano iliyopita kulikuwa na kitchen party ya binti ambaye ana matatizo ya akili, na jana ilikuwa ndio harusi yao ambapo yeye na mume wake wote wana matatizo ya akili.
Team ya Hekaheka ilikua ndani ya sherehe hiyo kushuhudia tukio hilo la aina yake ambalo lilikuwa na wageni wengi kabisa ambao walitaka kushuhudia.
Dada wa Bi harusi amezungumza jinsi maharusi hao walivyokutana, anasema ndugu wa pande zote mbili waliridhia waoane licha ya wote kuwa na tatizo la akili.
Bibi harusi mwenyewe kazungumza na kusema moja ya mipango yao ni kuwa na mtoto mmoja kwenye ndoa yao.
Hii hapa Hekaheka yote mtu wangu ..
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE