Kuna stori nadra kuzisikia katika Masikio yako kama hii inayotokea leo February 25, 2018 Serikali ya Singapore ambapo imetoa pesa zilizobaki katika bajeti ya mwaka 2017 kwa raia wake wote wenye umri wa zaidi ya miaka 21.
Raia wote wenye umri wa zaidi ya miaka 21 wataongezewa kiwango cha dola 100 hadi 300 katika mishahara yao.
Bajeti iliyopangwa na kutolewa kwa mwaka 2017 ilitumiwa na kiwango kikubwa cha pesa hakikutumika. Waziri wa fedha wa Singapore Heng Swee Keat amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuona kuwa bajeti ilikuwa kubwa.
Waziri wa fedha amesema kuwa serikali ya Singapore inatumikia raia wake na kuwa na lengo la maendeleo kwa kila raia wake. Ikumbukwe kuwa Singapore ilitoa kiwango cha dola 100 hadi 800 kwa raia wake mwaka 2011.
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi