Top Stories

Watu 10 wanashikiliwa na Polisi kwa kumkashfu JPM

on

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia Wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Stella Maris na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba kwa tuhuma za kumkashfu Rais John Magufuli na kuhamasisha maandamano ya April 26.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mtwara Lucas Mkondya akizungumza na waandishi wa habari amesema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp na Telegram kumkashfu Rais na kuhamasisha maandamano hayo.

“Ninatoa onyo watu wajiepusha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kusababisha uvunjifu wa sheria za nchi. Watuhumiwa wote tunawashikilia kwa upelelezi zaidi,” -Mkondya

Alichozungumza Fatma Karume baada ya kushinda urais TLS

 

Soma na hizi

Tupia Comments