Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limefanya mkutano na waandishi wa habari na kuitangaza habari njema kuhusiana na jezi za Taifa Stars, TFF leo wameingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya vifaa vya michezo ya Romario Sports 2010 Ltd.
Mkataba huo umelenga katika kutaka kuzipatia vifaa timu zote za taifa za Tanzania sambamba na kutoa mipira 600, mkataba huo umesainiwa na muwakilishi wa kampuni ya Romario Sports Minhaal Dewji pamoja na Rais wa TFF Wallace Karia huku ukishuhudiwa na Katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao.
Hiyo itakuwa ni habari njema kuelekea fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2019 ambapo Tanzania inashiriki, hivyo mashabiki watapata jezi original za Taifa Stars kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali kulikuwa hakuna jezi za Taifa Stars zinazouzwa mtaani zaidi ya walizokuwa nazo wachezaji.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega