Michezo

Siku 224 ameshindwa kuzitumia vizuri Obrey Chirwa, Azam FC yamtema

on

Kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2019/2020, club ya Azam FC ambayo imeanza kuonesha dhamira yake ya kuboresha kikosi kwa kusajili wachezaji mbalimbali, leo imetoa list ya wachezaji inaowaacha baada ya msimu wa 2019/2020 kumalizika.

Wachezaji hao saba walioachwa na Azam FC baada ya mikataba yao kumalizika ni Obrey Chirwa, Joseph Kimwaga, Daniel Lyanga, Enock Atta, Tafadzwa Kutinyu, Stephen Kingu na Ramadhan Singano ‘Messi’ uongozi wa Azam FC imewatikia kila la kheri wachezaji hao.

Chirwa anaachwa baada ya kudumu na club hiyo kwa siku 224 toka ajiunge nayo November 8 2018 kama mchezaji huru, Azam FC pamoja na kuachana na wachezaji hao saba, hadi sasa tayari imewasajili na kuwaongezea mikataba wachezaji Mwadini Ally, Benedict Haule, Braison Raphael, Iddi Seleman ‘Nado’ na kuingia mkataba na aliyekuwa kocha wa KMC Etienne Ndairagije.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments