Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imetoa habari njema kwa wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu nchini Tanzania kwa kuandaa shindano kwa wanachuo Tanzania Bara na visiwani kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi ambapo kushiriki kwake ni bure na kutakuwa na zawadi mbalimbali.
Akizungumza na waaandishi wa habari Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu ya mamlaka hiyo Nicodemus Mkama amesema kuwa shindano hilo ni kuwawezesha wanafunzi hao wa Vyuo Vikuu kupata fursa ya kupata elimu ya masoko ya mitaji na kuwawezesha kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa njia endelevu wakati wakiwa chuoni.