Michezo

MO Salah kapiga kijembe shirikisho la soka Misri, baada ya kugundua halijampigia kura The Best FIFA

on

Shirikisho la soka nchini Misri (EFA) limeiandikia barua FIFA kuomba ufafanuzi kuhusiana na kura yao ya tuzo ya The Best FIFA kutoonekana kitu ambacho kimempelekea staa wao Mohamed Salah anayeichezea Liverpool ya England kuona kama nchi yake inataka kumfanya aondoe mapenzi na taifa lake.

Kwa kawaida kura za kumchagua mchezaji bora wa FIFA wa mwaka huwa zinapigwa na makocha wa timu za taifa na manahodha na kuwasilishwa FIFA kupitia shirikisho la soka la nchi husika lakini kwa upande wa kura za Misri haijaonekana imeenda wapi wakati kulikuwa na MO Salah katika tuzo hizo, kitu ambacho kimeleta wasiwasi.

Inadaiwa kuwa MO Salah hajakichukulia poa kitendo hicho na badala yake ameandika ujumbe unaotafsiriwa kama dongo kwa shirikisho lake baada ya kushindwa kumpigia kura “Vyovyote wafanyavyo kwa ajili ya kujaribu kutaka kuondoa mapenzi yangu kwa Misri, hawatafanikiwa” huo ni ujumbe uliopo katika profile ya twitter ya Mohamed Salah kwa sasa.

Hata hivyo shirikisho la soka nchini Misri (EFA) limejitetea kwa kudai kuwa nahodha wao Ahmed Elmohamady na kocha wao Shawky Gharib walimpigia kura mchezaji huyo lakini hawajui kwa nini kura zao hazijaonekana katika upigaji kura, shirikisho la soka Misri limeomba ufafanuzi kutoka FIFA kwa nini kura yake ya The Best FIFA Award haijaonekana.

VIDEO: Antonio Nugaz kaanza na Mbwembwe Yanga “Yanga unyonge kwisha”

Soma na hizi

Tupia Comments