Michezo

Mwacheni Salamba achukue viatu vya Ever Banega kwa ajili ya watoto wake

on

Inawezekana mshambuliaji kinda wa Simba SC Adam Salamba kutokana na kejeli zinazoendelea katika mitandao ya kijamii kwa uamuzi wake wa kwenda kumuomba viatu baada ya game nahodha wa Sevilla Ever Banega, wengi wameupokea tofauti na inawezekana ni kitu nadra sana kuonekana katika soka la Tanzania.

Salamba kucheza dhidi ya mchezaji kama Banega ni kitu kikubwa na historia katika maisha yake ya soka, kitendo cha kuomba viatu vya Banega baada ya game baadhi ya watu mitandaoni wamekipokea tofauti lakini ni kitendo cha kawaida na kimewahi kutokea katika soka mara kadhaa.

CV ya Banega ni kubwa sana ukilinganisha na Salamba, Banega ana muda mchache wa kucheza soka wakati Salamba ana muda mrefu kutokana na umri wao, hii game ya Simba SC vs Sevilla ni game ya kihistoria sio tu kwa Tanzania ila hata kwa Salamba mwenyewe, inawezekana wengi wakawa hawamfahamu Banega labda ndio maana wanambeza Salamba, kama ambavyo wenye uelewa mkubwa wa soka hawashangai, Salamba ni kumbukumbu kubwa kwake na kwa ajili ya watoto wake kuja kuona kama baba yao amewahi kucheza dhidi ya Staa kama Banega.

Ni kitu cha kawaida kwa wachezaji wengi duniani inapotokea anacheza na mchezaji wa kiwango cha juu au rafiki yake basi hubadilishana jezi kama kumbukumbu au ishara ya urafiki wao, mchezaji kama Banega inawezekana aliombwa na wachezaji wengi wa Simba jezi yake, hivyo Salamba akaona ili kubaki na kumbukumbu ya Banega aombe kiatu kama kumbukumbu.

Banega mwenye umri wa miaka 30 ana CV kubwa anacheza timu ya taifa ya Argentina kikosi kimoja na mchezaji bora mara tano wa dunia Lionel Messi na alikuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichoongozwa na Lionel Messi katika fainali za Kombe la dunia 2018 zilizochezwa Urusi, Banega amecheza timu kama Valencia, Atletico Madrid na Inter Milan vilabu ambavyo ni wachezaji wachache wa Afrika wamewahi kupata nafasi na ndoto ya wachezaji wengi duniani.

Hivyo haishangazi kwa Salamba kuomba viatu hiyo ni kumbukumbu kwake, kwa mchezaji kama Salamba anayecheza Simba ana uwezo wa kununua kiatu kipya kila mwezi kwa ajili ya game ila kuomba kwa Banega ni kumbukumbu kwake, Mohamed Hussein amechukua jezi ya Banega wakati Salamba kaomba viatu kama kumbukumbu kwake.

Tukio kama hili liliwahi kutokea 2013 nchini Morocco December 18 2013 katika mchezo wa club Bingwa dunia kati ya Atletico Mineiro ya Brazil iliyokuwa na Ronaldinho dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco na mchezo kumalizika Atletico Mineiro ikifungwa 3-1, baada ya game wachezaji wa Raja Casablanca walivigombania viatu alivyokuwa amevaa Ronaldinho na jezi, yupo aliyechukua jezi na wengine wakagawana kiatu kimoja kimoja kama kumbukumbu kwao waliwahi kucheza dhidi ya Ronaldo, sio kitu cha kawaida na nadra sana kupata nafasi ya kucheza dhidi ya wachezaji wenye heshima kubwa duniani.

Mapokezi ya Sevilla Tanzania waliokuja kukipiga na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments