AyoTV

VIDEO: Kauli ya Yanga kuhusu stori za kocha wa Zesco kutua Yanga

on

Baada ya kuenea kwa stori za klabu ya Yanga kutaka kumleta kocha wa klabu ya Zesco ya Zambia George Lundamina, kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit ametoa tamko rasmi kuhusu kuenea kwa taarifa hizo katika mitandao ya kijamii.

“Wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga kumekuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa kuna ujio wa kocha mpya Yanga na benchi la ufundi jipya, napenda kukanusha taarifa hizo hadi hivi sasa timu ya Yanga inaongozwa na becnchi la ufundi lilelile chini ya Hans van Pluijm”

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments