Michezo

Anachofikiria Mbwana Samatta kuhusu Taifa Stars kwa sasa

on

Kuelekea fainali za michuano mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019 maarufu kama AFCON, nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, kupitia ukurasa wake wa instagram ameuliza swali.

Samatta ambaye ni nahodha wa kikosi cha Taifa Stars kinachopambania kucheza fainali za AFCON 2019, ameuliza swali kwa mashabiki kuhusiana wao wanadhani nini kifanyike Taifa Stars icheze fainali za mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019.

Samatta ameandika hivi “Hivi ukipata nafasi ya kushauri chochote ambacho kinaweza kuifanya ‘taifa stars’kupata tiketi ya afcon mwakani unadhan ungeshauri jambo gani? Nini kifanyike? Sina maana ushauri utafatwa ama la lakini tuongelee tu hili jambo hapa lets start”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Tanzania ipo nafasi ya pili sawa na Lesotho katika Kundi L lenye timu za Lesotho, Uganda na Cape Verde na kila kundi ni timu mbili zitafuzu, hivyo ili afuzu ni lazima amalize katika Kundi hilo akiwa nafasi mbili za juu.

AyoTV ilivyomnasa staa wa zamani wa Liverpool Airport KIA

Soma na hizi

Tupia Comments