Michezo

Kwa mara ya kwanza Bakhresa katoa ndege yake iwabebe wachezaji

on

Kwa mara ya kwanza mfanyabiashara na mmiliki wa club ya Azam FC Said Salim Bakhresa aliamua kuwasafirisha wachezaji wa timu yake ya Azam FC kutoka Bukoba hadi Dar es Salaam kwa ndege yake binafsi.

Mtandao wa muandishi wa habari za michezo wa BinZubery umeripoti kuwa Bakhresa aliamua kutumia ndege yake binafsi ambayo huwa anatumia na familia yake kuwasafirisha wachezaji wa Azam FC walioitwa Taifa Stars na kocha wao Hans van Plujm na Dr wa timu Mwanandi Mwankemwa.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 13, iliwasafirisha Aggrey Morris, Yahaya Zayd, Mudathir Yahya, Abdallah Kheri, Salum Abubakar pamoja na Nico Wadada aliyeenda kujiunga na timu yake ya taifa ya Uganda na Tafadzwa Kutinyu aliyejiunga na Zimbabwe

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments