Michezo

Watanzania waliolala masikini na kuamka wakitangazwa mamilionea

on

Washindi wa Sh Mil. 825 za Jackpot Bonus SportPesa waelezea walivyoshinda
Watanzania wawili wa waliofanikiwa kuibuka washindi wa Tsh Shilingi 825, 913, 640 za Jackpot ya SportPesa jana wamewasili jijini Dar es Salaam na wanatarajiwa kukabidhiwa mamilioni yao kesho August 27.

Washindi hao ni Kingsley Simon Pascal kutoka Biharamuro, Kagera na Magabe Matiku Marwa wa Mugumu, Serengeti, washindi hao wawili wamegawana Shilingi Mil.142 kila mmoja kati ya Mil.825 walizoshinda baada ya wote wawili kushinda ubashiri wao mechi 13 wikiendi hii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Pascal ambaye ni mtumishi wa umma alisema kuwa alianza kubashiri na SportPesa tangu mwaka 2017 kabla ya wikiendi iliyopita kushinda, Pascal alisema kuwa huo ni ushindi wake wa kwanza kuupata tangu aanze kubashiri na kushinda, hivyo anajisikia furaha.

” Jumatatu ndiyo nimeanza kuamini kuwa nimeshinda rasmi licha ya kupewa taarifa na SportPesa nikiwa nyumbani Kagera, Niwaambie Watanzania kuwa hili jambo la ukweli kabisa na mimi ndiye mshindi halari wa jackpoti hii kubwa ya SportPesa”

VIDEO: Niyonzima kaeleza kilichotokea kati yake na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments