Michezo

Rais wa FUFA nchini Uganda kajiweka pembeni, FIFA ifanye uchunguzi

on

Baada ya May 30 2017 mbunge wa jimbo la Makindye Magharibi Allan Ssewanyana kupeleka tuhuma FIFA kuwa Rais wa shirikisho la soka nchini Uganda Moses Magogo aliuza kinyume na taratibu tiketi 177 za Kombe la Dunia 2014 tofauti na ilivyoelekezwa na FIFA.

Kwa kawaida FIFA hutoa tiketi za fainali za Kombe la Dunia kila zinapofanyika katika mashirikisho ya soka wanachama wake kwa lengo la shirikisho husika kuwauzia raia wa nchini kwake ambao watapenda kwenda kuangalia fainali hizo ila Magogo atuhumiwa kuuza tiketi hizo nje ya Uganda.

Allan Ssewanyana ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo ndio alipelekea tuhuma hizo ambazo zimepelekea Moses Magogo kutangaza kujiweka pembeni kwa kipindi cha miezi miwili ili kupisha uchunguzi na nafasi yake itakaimiwa na makamu wa Rais wa kwanza wa FUFA.

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments