Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Tanzania na Rwanda hakuna mbabe katika wiki ya FIFA

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo ilikuwa Kigali Rwanda kucheza mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda, mchezo huo ulikuwa unakutanisha timu ambazo hazijaachana sana katika viwango vya FIFA, Tanzaia ikiwa nafasi ya 135 na Rwanda ikiwa nafasi ya 30.

Taifa Stars iliingia katika mchezo huo kuimarisha zaidi safu yao ya ushambuliaji kuelekea mchezo wao dhidi ya Sudan kwani kwa hivi karibuni Taifa Stars ikiwa chini ya Kocha Etienne Ndairagije imekumbwa na ukata wa magoli ikicheza jumla ya michezo mitano jumla pamoja na CHAN na FIFA World Cup ya kufuzu ikifunga jumla ya magoli 2 tu!! na imeruhusu kufungwa magoli 3.

Kwa leo Stars ilionekana kuimarika zaidi katika mchezo huo kwani licha ya kumaliza mchezo bila kufungana (0-0), Taifa Stars ilionekana kutengeneza nafasi zaidi, Taifa Stars itaendelea kuwa Rwanda ikijifua kabla ya kwenda Khartoum Sudan kucheza mchezo wa kufa na kupona wa kuwania kufuzu kucheza fainali za CHAN 2020 zitakazofanyika nchini Cameroon, Stars walipoteza mchezo wao wa kwanza 1-0 dhidi ya Sudan.

VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA

Soma na hizi

Tupia Comments