Tume ya Uchaguzi wa Zambia imemtangaza Kiongozi wa Upinzani, Hakainde Hichilema kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais uliofanyika Alhamisi iliyopita.
Rais aliyekuwepo Edgar Lungu, ametishia kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo, hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa, Wafuasi wa Hakainde Hichilema na Chama chake cha United Party for National Development, UPND walijimwaga katika mitaa ya mji mkuu Lusaka na kushangilia, ilipodhihirika kuwa mgombea wao alikuwa akielekea kwenye ushindi, hii ikiwa mara yake ya sita kujitosa katika kinyang’anyiro cha Urais wa Zambia.
Alfajir ya leo, mbele ya waandishi wa habari na wadau wengine, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia Esau Chilu, baada ya matokeo kutoka majimbo 155 kati ya 156, amemtangaza Hichilema kuwa mshindi.