Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Chelsea kwa sasa haina kocha baada ya kumfukuza kazi kocha wao mkuu Jose Mourihno.
Headlines za sasa zimemgeukia kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ulolanzi Guus Hiddink ambaye ametajwa kukaimu nafasi ya Mourihno na tayari amesafiri kwa ndege leo kwenda kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo.
Hiddink, aliwahi kunoa Chelsea na kuwasaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2009, lakini bado hawajafikia makubaliano ya mkataba.
Pia Hiddink alishinda mataji sita ya ligi ya Uholanzi na Kombe la Ulaya akiwa meneja wa PSV Eindhoven ya Uholanzi katika vipindi viwili.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.