Top Stories

Hifadhi ya Mikumi kuboreshwa

on

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Hifadhi ya Taifa Mikumi ni miongoni mwa hifadhi iliyotengewa fedha za Mradi wa Kusimamia na Kuendeleza Utalii Nyanda za Juu Kusini (REGROW) hivyo inatarajiwa kuwa na miradi ya kimkakati itakayosaidia kuongeza idadi ya watalii katika eneo hilo.

Amesema hayo alipotembelea hifadhi hiyo katika Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro leo.

Masanja ameongeza kuwa mradi wa REGROW umetenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 69 zitakazogawanywa kwenye Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udzungwa na Ruaha na Nyerere imetengewa Dola za kimarekani milioni 37.7.

Fedha za REGROW zitatumika kununua mitambo, vifaa vya doria, vitendea kazi vya ofisi, kuboresha maeneo mbalimbali kama kujenga hostel, picnic sites, bandaz, camp sites, rest houses, ranger posts na viwanja vya ndege.

Aidha, Masanja amewahimiza watanzania kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kutalii na pia kuwekeza ndani ya hifadhi hiyo.

Soma na hizi

Tupia Comments