Katika ukanda wa Afrika Hifadhi ya Mpanga Kipengere ndiyohifadhi pekee yenye idadi kubwa ya Maanguko ya Maji yenye muonekano tofauti na wa kuvutia;Hifadhi hiyo inayosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA); ina maanguko ya Maji zaidi ya 15 ndani ya Hifadhi.
Maanguko hayo yana tiririsha maji wastani wa kimo cha kuanzia mita 20 hadi 400 kutoka juu hadi chini ambapo yanatengeneza mabwawa asilia ya kuogelea – natural swimming pool. Yapo yanayoanguka kwa mfumo wa ulalo – horizontal falling, mengine kama nguzo au zigzag na mengine yanadondoka katika mfumo unaotengeneza ghorofa ambapo yanatengezeza ghorofa yenye floor 10.
Hivyo Juni 16 ya kila mwaka Dunia husherehekea siku ya manguko ya maji Duniani. Ujumbe wa mwaka huu kutoka hifadhi ya Mpanga Kipengere ni “Linda Maanguko ya Maji kukabiliana na mabadiliko ya ya tabia nchi”. Ikiwa maanguko ya maji yanayovutia zaidi hifadhini ni Kimani, Lyamakunohila, Merere na Nyaugenge. Mengine ni Kipengere, Mwamba, Itagho na Nyaluliva.
Hifadhi ya Mpanga Kipengere inapatikana katika Wilaya za Wanging’ombe, Makete kwenye Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Mbarali Mbeya. Hifadhi ilianzishwa mwaka 2002 kwa lengo kuu la uhifadhi wa vyanzo vya maji na bioanuai.