Mix

Maamuzi mengine ya Mahakama Kuu Dar kuhusu ishu ya Chenge na ESCROW.. (Audio)

on

IMG_1119

Ishu ya ESCROW ni kama kuna watu wengi walianza kuisahau hivi, imerudi leo kwenye masikio ya watu ambapo tunakumbuka kuna list ya Mawaziri na Wenyeviti wa Kamati za Bunge walisimamishwa baada ya kutajwa kuhusika na mgao wa Bil. 300 zilizokuwa kwenye account ya ESCROW.

Mbunge Andrew Chenge alikuwa mmoja ya waliotajwa kuhusika pia, ishu ikapelekwa Kamati ya Maadili na baadae Mbunge huyo akapeleka ombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ili kuzuia kuhojiwa na Kamati hiyo.

IMG_1121

leo June 26 2015 ripoti kutoka Mahakamani inasema Mahakama hiyo imetupilia mbali Ombi hilo kwa kuwa imeona haikuwa na Mamlaka ya kuzuia Shauri hilo, na walichokiona ni kwamba Chenge alikuwa na njia mbadala kushughulika na ishu hiyo badala ya kukimbilia Mahakamani.

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments