Michezo

Hii hapa ni rekodi nyingine kubwa aliyoivunja Lionel Messi

on

IMG_8980.JPG

Akiwa na miaka 27, Lionel Messi bado ana miaka zaidi ya mitatu ya kucheza soka katika kiwango cha juu, na kila siku anavunja na kuweka rekodi mpya katika medani za soka.

Baada ya wiki mbili zilizopita kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wa ligi ya mabingwa wa ulaya akiwa kamfikia Raul Gonzales kwa kufikisha magoli 71 katika michuano hiyo.

Leo hii Lionel Messi amevunja na kuweka rekodi mpya ya ufungaji wa magoli kwenye ligi kuu ya Hispania.

Kabla ya mchezo dhidi ya Sevilla leo hii Messi alikuwa na jumla la magoli 250 kwenye ligi hiyo, hivyo alikuwa anahitaji goli moja tu kumfikia gwiji wa Atletico Bilbao Telmo Zarra ambaye alikuwa ndio mfungaji bora wa La Liga wa muda akiwa na jumla ya magoli 251.

Lakini mpaka kipenga cha mwisho kipopulizwa Lionel Mess kwa mara nyingine alikuwa anajiandika kwenye vitabu vya histori – akifunga hat trick na hivyo kuivunja rekodi ya Zarra kwa kutimiza jumla ya magoli 253.

Pongezi kwa Lionel Messi kwa kuwa mfungaji bora wa La Liga wa muda wote.

IMG_8987.JPG

Tupia Comments