Michezo

Hii hapa sababu ya Ronaldo kushangilia kwa style ya ‘Hulk’ kwenye fainali dhidi ya Atletico

on

article-2642644-1E2F06B700000578-447_634x419.jpg

Ripoti nchini Hispania zinasema kwamba Cristiano Ronaldo alivua jezi yake mbele camera wakati akishangilia goli lake kwenye mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kwa sababu alikuwa akirekodi filamu yake binafsi.

Nahodha huyo wa Ureno alifunga penati katika dakika za mwisho za extra time na kuhakikishia timu yake ubingwa wa 10 wa ulaya kwa ushindi 4-1 dhidi ya Atletico Madrid, na baada ya kufunga penati hiyo alishangilia huku akivua jezi yake na kuonesha misuli yake mbele ya camera zilizokuwa zimemzunguka.

Ushangiliaji wake ulizua maswali kutokana kwamba goli lake halikuwa na umuhimu mkubwa kwa sababu ilionekana wazi Madrid walikuwa wameshaweka kombe kibindoni, lakini ripoti nchini Spain zinasema kwamba alifanya vile makusudi ili watu wake waliokuwa uwanjani wakirekodi filamu yake kwa siri wapate picha nzuri.

Inaaminika Ronaldo anatengeneza filamu aliyoipa jina la ‘Ronaldo: The Movie’, lakini mpaka sasa hakuna chochote kilichothibitishwa na Ronaldo mwenyewe kuhusu taarifa hizo.

Tupia Comments