Top Stories

“Hii kodi tumeiweka kwa ajili ya wenye uwezo” Zungu

on

Hoja kuhusu viwango vya tozo za miamala ziko juu ni kweli yaani Laki moja inatafutwa kwa mbinde halafu ada inakatwa mara tatu, ndio maana Rais Samia ametoa maagizo kwamba litizamwe wapi tulipokosea” Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala 

“Hii kodi tumeiweka kwa ajili ya wenye uwezo, kati ya Watu Mil. 50 wanaomiliki line za simu, Watu Mil. 20 tumewatoa hawalipi hii kodi, wanaolipa ni Mil. 30 ambao tunaamini wana uwezo kiasi na tunajuaje wana uwezo ni kwa kupitia TCRA” Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala 

“Tukisema Tshs. 50 kwa Watu Mil. 30 (wanaolipa tozo za simu) tunapata Bil. 540. Tukiweka Tshs 100 tunapata Tril. Moja na Bil. 80 haya ni mapato ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya Nchi yetu” Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala 

“Kuwa na ada ya simu ni uzalendo leo hatuandiki barua, hatuna gharama ya stempu, leo Mtu yupo Mwanza anauliza Soko la Pugu ni shilingi ngapi, anauliza soko la samaki ni shilingi ngapi, hii ni nafasi nzuri tuwe na kodi ya uzalendo”———Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala 

MTOTO MDOGO WA GIFT ALIYEUAWA ASIMULIA ALICHOAMBIWA NA BABA YAKE KABLA HAJAFA, MAMA ATOA YA MOYONI

Soma na hizi

Tupia Comments