Michezo

Hii ndio adhabu ya FIFA kwa Jamal Malinzi baada ya kumkuta na hatia

on

Kamati huru ya maadili ya FIFA imemkutana na hatia Rais wa zamani wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, ambaye amekuwa na tuhuma za makosa mbalimbali ya matumizi ya fedha za FIFA.

November 8 2019 FIFA imemfungia Jamal Malinzi kwa miaka 10 kutojihusisha na soka na kutakiwa kulipa Tsh Bilioni 1.1 (CHF 500,000) kama faini, FIFA baada ya kujiridhisha na kumkuta na makosa ya matumizi mabaya ya fedha za FIFA zilizotolewa kwa ajili ya uendeshaji ndani ya TFF.

Kutoka kushoto ni Selestine Mwesigwa na Jamal Malinzi

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na FIFA umebaini kuwa Malinzi alitumia pesa za FIFA, CAF na TFF kinyume na taratibu katika kipindi cha 2013 hadi 2017 ikiwemo kugushi nyaraka kwa kamati ya utendaji na kujilipa Tsh milioni 454 kwa madai kuwa alikuwa kaikopesha TFF kinyume na taratibu.

Hata hivyo Jamal Malinzi pamoja na aliyekuwa katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa bado wanashikiliwa na Polisi kesi yao ikiwa Mahakamani kwa tuhuma mbalimbali (20) ikiwemo kugushi nyaraka, utakatishaji fedha na matumizi mabaya ya madaraka.

TOP 5: Samatta anaondoka UEFA Champions League na rekodi hizi

Soma na hizi

Tupia Comments