Top Stories

Hii ndio safu mpya ya Uongozi Baraza la Wanawake CHADEMA

on

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, amechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), baada ya kupigiwa Kura za Ndio 317 kati ya Kura 324.

Matokeo ya Uchaguzi huo yametangazwa leo Disemba 13, 2019, ambapo kupitia ukurasa wa Twitter wa chama hicho ukatoa mchanganuo wa Mwenyekiti pamoja na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara na Zanzibar.

“Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) ulioanza jana asubuhi, umemalizika asubuhi hii ambapo umemchagua Halima Mdee kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa” 

Aidha katika Uchaguzi huo Hawa Mwaifunga, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Tanzania Bara, huku Sharifa Suleiman, akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

NDEGE ILIYOKAMATWA CANADA ILIVYOACHIWA NA KUONDOKA KWENDA MWANZA

Soma na hizi

Tupia Comments