Michezo

Hiki ndicho walichokisema Yanga baada ya TFF kumsimamisha Okwi.

on

yangaUongozi wa klabu ya Yanga umeweka hadharani ukweli kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji kutoka Tff  imemzuia kuichezea Yanga mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.

Yanga ilikamlisha usajili wa mshambuliaji huyo tangu Disemba 15 mwaka 2013, na kupata hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC) ambayo iliwasilishwa TFF pamoja na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom.

itcHii ndiyo Hati ya Usajili wa Emmanuel Okwi kama inavyoeneka kwenye system ya CAF

Baada ya kukamilisha zoezi hilo TFF ilipitisha jina lake kwa kutupatia leseni no: 921225001 ambayo i;imruhusu Okwi kuichezea Yanga na kisha kulituma CAF Disemba 31, 2013 kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika  ambapo CAF nao walimuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Yanga kwa mashindano hayo.

Siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji  Tff walimzuia mchezaji huyo kuichezea Yanga wakati taarifa inasema kuwa alikua ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa mchezaji halali wa Young Africans.

Kuna maswali bado wanajiuliza baadhi ya watu ikiwa ni pamoja na kwamba walikuwa wapi Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji kujiridhisha juu ya usajili ambao ulishakamilika tangu Disemba 15 2013?

Ambapo wamekuja kutoa maamuzi hayo mwezi mmoja na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa, ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom??

Source:www.youngafricans.co.tz

Tupia Comments